MAN UNITED VS REAL MADRID: SIFA NA UWEZO WA KILA TIMU NDIYO MUAMUZI WA MECHI YA LEO
Real Madrid hivi karibuni wameshinda mara mbili mfululizo dhidi ya mahasimu wao Barcelona, lakini wanasubiriwa na mtihani mwingine mgumu leo pale Old Trafford.
Kikosi cha Sir Alex Ferguson kiliweza kulazimsisha sare ya 1-1 wiki tatu zilizopita kwenye uwanja wa Bernabeu, hivyo Mourinho na Madrid yake leo itakuwa na kazi kushambulia zaidi ili kuweka hai matumaini ya kupita.
Hivyo inamaamisha leo hii kutakuwa na vita kubwa sana katika washambuliaji wa Madrid dhidi ya walinzi wa lango la United. Lakini vita haitokuwa hiyo tu - hivi ni vitu vitano vingine vitakavyoamua nani katika ya magwiji hawa wa soka barani ulaya anaendlea kwenye hatua ya robo fainali.
ANGEL DE MARIA VS MABEKI WA UNITED
Angel Di Maria, muargentina aliye kwenye fomu nzuri sasa hivi, amekuwa akipangwa kwenye kila mechi muhimu wakati Madrid wakitumia mfumo wa kuchezesha washambuliaji watatu. Akiwa anahama kutoka winga moja mpaka nyingine kuhakikisha Madrid inatamba.
Katika mechi ya kwanza wiki tatu zilizopita, Di Maria alitoa krosi safi iliyomfikia Ronaldo na kuwa goli - krosi ikitokea upande wa kushoto ambao ndio Ronaldo anaanzaga kwenye mechi.
Di Maria na Ronaldo wanaweza kuwa upande wowote wa uwanja muda wowote. Ronaldo kwa hakika atatolewa macho zaidi, lakini Di Maria na krosi zake, uharaka na ujuzi wa kupenya yeye mwenye au mipira yake unaweza ukawa hatari kubwa kwa upande wa Man United.
Wapinzani wa Di Maria watakuwa mabeki wa pembeni wa United Evra na Rafael, na ikiwa Di Maria atacheza vizuri sana kwa hakika hali haitokuwa salama langoni mwa Mashetani wekundu. Ni mmoja ya watu wanaoweza kuamua mechi hii.
VIUNGO WA ULINZI WA MADRID VS WASHAMBULIAJI WA UNITED
Kuna taarifa kwamba Ferguson anaweza asimuanzishe Wayne Rooney leo hii, inaweza ikawa kweli au ni mbinu tu za mscotland huyo kuwachanganya Real Madrid.Vyovyote itakavyokuwa leo, tunafahamu kwamba Real Madrid hawapaswi kuruhusu nyavu zao kuguswa usiku wa leo. Kuruhusu goli hasa mapema itamaanisha inabidi wacheze sana na kufunga mabao mawili ili kuweza kupita. Hivyo ushirikiano mzuri wa beki ya madrid utakuwa mchango muhimu sana. Walinzi wa kati na viungo wakabaji wanapaswa kuwa makini zaidi.
Mjerumani Sami Khedira mhispania Xabi Alonso mara nyingi huwa wanaanza pamoja na wanatengeneza ushirikiano mzuri sana kama viungo wa ulinzi mbele ya ukuta. Kazi yao na kuwalinda walizni wanne wa nyumana kuunganisha safu ya ulinzi na ushambuliaji. Pamoja na uwezo wake wa kuzuia, Alonso anatambulika kwa pasi znuri na zenye maana.
Khedira na Alonso ni wazuri sana kwenye eneo hilo, lakini United wana washambuliaji hatari. Machaguo kama Robin Van Persie, Rooney, Danny Welbeck na Chicharito.
Wikiendi iliyopita, Shinji Kagawa alifunga hat-trick katika ushindi wa United 4-0 dhidi ya Norwich City. Pia kuna winga wazuri kama vile Nani, Ashley Young na Valencia ambao kama wanakutana safu ya ulinzi isiyokuwa imara wanaweza wakaleta madhara makubwa.
MICHEAL CARRICK VS OZIL
Cristiano Ronaldo, Robin van Persie na wafungaji wengine wanaweza kuwa wanatajwa sana kwenye vyombo vya habari. Japokuwa viungo wanaweza kuwa waamuzi wa hii mechi.
Mjerumani Mesut Ozil usiku zote huwa anacheza kama kiungo mchezashaji wa Real Madrid, akicheza nyuma ya Karim Benzema au Gonzalo Higuain. Au iwe tofauti meneja Jose Mourinho achague kumpanga Kaka au Luka Modric kuanza, lakini ishara zote leo zinaonyesha Ozil ataanza kwenye mechi leo.
Mpinzani wake mkuu atakuwa kiungo aliye kwenye fomu msimu wa United Micheal Carrick, ambaye hucheza nyuma kidogo ya kiungo cha United huku akicheza part kubwa ushambuliaji wa United.
Ozil inawezekana akawa anaonekana bora zaidi kwenye levo ya kimataifa zaidi ya Carrick, lakini mchango wa muingereza Carrick kwenye timu ya United hasa msimu huu umekuwa muhimu sana. Upinzania baina ya wawili hawa unaweza ukaaamua mechi.
MBINU(FERGIE VS MOURINHO)
No comments:
Post a Comment