HII NDIO MIFUMO YA TIMU ZOTE ZA LIGI KUU NA NA SABABU KWANINI MAKOCHA WANAITUMIA
KILA kocha wa soka ana falsafa yake ya ufundishaji, lengo likiwa kushinda kila mechi na kufikia malengo ambayo amejiwekea.
Pia, katika soka kuna mifumo mingi na tofauti ya uchezaji ambayo huendana sana na aina ya wachezaji wa timu husika.
Baadhi ya mifumo ambayo imezoeleka katika soka la sasa ni 4:4:2, 4:3:3 na 4:5:2.
Makala haya yanakuchambulia timu zote 14 zinashiriki Ligi Kuu Tanzania Bara na mifumo yake.
YANGA SC
Mfumo; 4:4:2
YANGA hucheza mfumo wa 4-4-2, lakini Mholanzi Ernie Brandts amekiri kuwa mambo yanapokuwa magumu hubadilika na kucheza 4-3-3.
"Kwa kawaida huwa tunacheza 4-4-2. Lakini mambo yanapoharibika tunalazimika kutumia fomesheni ya 4-3-3." Brandts anaeleza kuwa anapotumia mfumo wa 4-3-3 hushambulia zaidi kutokana nakucheza na washambuliaji watatu ambao ni Jerry Tegete, Said Bahanuzi na Himis Kiiza.
"Wakati tunapokuwa kwenye mfumo wetu wa 4-4-2 tunafanya yote kwa pamoja. Kushambulia na vile vile kujihami kufungwa kirahisi." anasema kocha huyo aliyevaa viatu vya Mbelgiji Tom Saintfiet aliyetupiwa virago na Yanga.
SIMBA SC
Mfumo; 4:3:3
MFARANSA Patrick Liewig ameeleza kuwa tangu ametua na kuanza kazi ya kukinoa kikosi cha Simba akichukua mikoba ya Mserbia Milovan Cirkovic ameona mfumo 4-3-3 ndio ambao Simba wameonyesha kufiti tofauti na 4-4-2.
"Nilipokabidhiwa timu nilijaribu kutumia mifumo tofauti. Lakini nafikiri 4-3-3 ni bora zaidi kwetu." anasema kocha huyo. Liewig anafafanua kuwa aina ya wachezaji ambayo wanaunda kikosi cha Simba ni sahihi kucheza mfumo wa 4-3-3 kuliko 4-4-2.
AZAM FC
Mfumo;4:3:3
MWINGEREZA Stewart Hall ambaye ni kocha mkuu wa timu hiyo amefichua kuwa hucheza 4-3-3, ingawa wakati mwingine hubadilika na kutumia 4-4-2.
"Mara kwa mara tunacheza 4-3-3, lakini wakati mwingine tunapaswa kubadilika kutokana na mpinzani wetu anavyocheza."
Stewart anaeleza kuwa anapobadilisha fomesheni hucheza 4-4-2.
"Kwa aina ya wachezaji ambao ninao kwa sasa, nafikiri mfumo sahihi kwetu kucheza ni 4-3-3." anasema kocha huyo aliyetemwa na kurejeshwa kwa
mara nyingine kukinoa kikosi hicho.
MTIBWA SUGAR
Mfumo; 4:5:1
MECKY Maxime ambaye ni kocha mkuu wa Mtibwa anasema hutumia mfumo wa 4:5:1, lakini wakati mwingine hubadilika na kucheza 4:3:2:1.
Mchezaji huyo wa zamani wa Mtibwa na Taifa Stars anaeleza kuwa lengo la kucheza 4-3-2-1 ni kutanua uwanja na kufanya mashambulizi mengi kusaka ushindi.
"Mara nyingi tunavyotumia mfumo wa 4-5-1. Tayari tumeshinda kwa hiyo tunataka kulinda ushindi wetu na kumiliki mpira." anasema kocha huyo.
COASTAL UNION
Mfumo; 4:3:3
KOCHA Mkuu, Hemed Morocco anasema hutumia mfumo 4-3-3 kwa lengo la kutanua Uwanja na kufanya mashambulizi yake kupitisha mipira pembeni ya uwanja.
"Nafikiri timu ambazo zinafanya vizuri duniani kwa sasa zinatumia zaidi mawinga wake kutengeneza ushindi. Pia, kwa aina ya wachezaji ambao ninao, nafikiri nalazimika kucheza 4-3-3." anasema Morocco aliyerithi mikoba ya Juma Mgunda aliyejiuzulu kukinoa kikosi hicho kwa shinikizo la wanachama na mashabiki wa mabingwa hao wa Ligi Kuu Bara 1988.
Coastal inawatumia mawinga wake wawili, Daniel Lyanga na Seleiman Kassim 'Selembe' ambao wana uwezo mkubwa pia wakufunga mabao.
JKT RUVU
Mfumo; 3:5:2
NI moja kati ya timu ambazo zinasifika kwa soka la pasi fupi na kushambulia kama nyuki. Soka la JKT Ruvu halitofautiani sana na la Kagera Sugar.
Kocha Charles Kilinda anasema hana mfumo maalum wakutumia isipokuwa hutegemea na timu ambayo anakabiliana nayo.
"Sina mfumo maalum wakutumia isipokuwa nacheza kulingana na mpinzani wangu anavyocheza na aina ya wachezaji wake."
Kilinda anafafanua kuwa mara nyingi hutumia mfumo wa 3-5-2, Pia, wakati mwingine hubadilika na kucheza 4-4-2.
KAGERA SUGAR
Mfumo; 4:4:2
MRANGE Kabange ambaye ni kocha msaidizi wa Kagera Sugar anasema kwa kipindi kirefu wamekuwa wakitumia mfumo wa 4-4-2.
"Ni mfumo ambao wachezaji wetu wameonyesha kuushika vizuri na kumudu tofauti na mifumo mingine tunapojaribu kucheza." anasema kocha huyo.
Kabange anafafanua maana ya kucheza mfumo huo ni timu iweze kucheza soka la pasi fupi.
"Falsafa yetu ni kucheza soka la pasi fupi. Kwa maana hiyo lazima tucheze tukiwa karibu. Mipira ya juu kwetu mwiko." anasisitiza.
RUVU SHOOTING
Mfumo; 4:5:1
KOCHA mkuu, Boniface Mkwasa anasema lengo lake kutumia mfumo huo ni kuiteka sehemu ya katikati ya Uwanja.
"Falsafa yangu kubwa ni kucheza na viungo watano katikati ya uwanja."
Mkwasa anasema anaamini akiweza kutawala sehemu ya kiungo inakuwa kazi rahisi kwa timu yake kujenga mashambulizi ya kusaka ushindi. Pia, anasema inapotokea timu yake imebanwa hubadilisha mfumo na kucheza 4-4-2.
OLJORO JKT
Mfumo; 4:2:3:1
KATIBU wa Oljoro, Alex Mwamgaya ambaye kwa sasa anashirikiana na kocha msaidizi, Fikiri Edward kukinoa kikosi hicho anasema timu hiyo anatumia mfumo wa 4-2-3-1.
"Nafikiri mfumo ambao tunatumia ni kwa ajili ya kujihami na vile vile kushambulia."
Mwamgaya anaeleza kuwa mabeki wanne na viungo wawili wakabaji kazi yao kubwa ni kuhakikisha timu hairuhusu bao kirahisi.
Anasema kazi ya viungo watatu ni kuunganisha timu kutoka nyuma na kwenda mbele kushambuliaji.
"Majukumu yao ni mawili, kutengeneza nafasi za kufunga na pia kufunga inapotokea nafasi."
TANZANIA PRISONS
Mfumo; 4:2:3:1
KOCHA mkuu, Jumanne Chale aliyeinoa African Lyon msimu uliopita, anasema wacheza mfumo wa 4-2-3-1.
"Lengo letu ni kuhakikisha hatufungwi kirahisi. Pia tunashambulia." Chale aliyerithi mikoba ya Stephen Matata aliyeipandisha timu hiyo Ligi Kuu msimu huu anaeleza kuwa mara nyingine hubadilika kutokana na timu anayokabiliana nayo.
"Wakati mwingine tulazimika kubadilika kulingana na mpinzani wetu."
Anasema anavyobadilika hucheza 4-4-2 na mara nyingine 4-3-3.
MGAMBO JKT
Mfumo; 5:3:2
KOCHA mkuu, Mohamed Kampira aliyerithi mikoba ya Stephen Matata anasema anatumia mfumo wa 5-3-2.
"Silaha yetu kubwa ni kushambulia na kurudi nyuma kwa pamoja kujilinda."
Kampira anaeleza kuwa lengo la kutumia fomesheni hiyo ni wasifungwe kirahisi, lakini timu yake ishambulie.
TOTO AFRICAN
Mfumo; 4:4:2
TANGU Toto imeanza kushiriki Ligi Kuu misimu mitatu iliyopita imekuwa ikitumia mfumo wa 4-4-2.
Kocha msaidizi, Athuman Bilali 'Bilo' anasema mfumo huo umekuwa rahisi kwao kulingana na aina ya wachezaji wanaounda timu hiyo.
"Kila mwalimu anatumia mfumo wake kulingana na aina ya wachezaji alionao." Bilo anaeleza ni vigumu leo ukaitaka Chelsea icheze kama Arsenal.
"Lazima kuwe na maandalizi. Huwezi kukurupuka usingizini na kubuni fomesheni. Leo tucheze 4-3-3, kesho 5-3-2." anasisitiza kocha huyo.
AFRICAN LYON
Mfumo; 4:4:2
MKURUGENZI wa Ufundi, Charles Otieno anasema timu hiyo inatumia mfumo wa 4-4-2. Lakini mambo yanapokuwa magumu hugeuka na kutumia 3-5-2.
"Fomesheni yetu ni 4-4-2, Lakini inapotokea kumeshikwa tunageuka na kutumia 3-5-2. Nafikiri kila mwalimu lengo lake ni kupata ushindi kila mechi."
Otieno anafafanua kuwa timu hiyo inapotumia mfumo wa 4-4-2 hushambulia na pia kujihami.
"Tunapogeuka na kucheza 3-5-2. Lengo letu huwa ni kushambulia kuliko kujilinda."
POLISI MORO
Mfumo; 4:4:2
KOCHA mpya, Adolf Rishard anasema tangu ameanza kazi ya kuinoa Polisi Moro anacheza katika mfumo wa 4-4-2.
"Mifumo ni mingi ya uchezaji, lakini inategemea sana na aina ya wachezaji ulionao." anasema kocha huyo aliyerithi mikoba ya John Simkoko aliyetupiwa virago na Polisi kushindwa kupata ushindi ngwe yote ya kwanza ya ligi.
Rishard anasema mfumo ambao anacheza ni 4-4-2 kulinga na aina ya wachezaji wanaounda timu yake.
"Kwa kiasi kikubwa fomesheni ya 4-4-2 imenipa mafanikio makubwa."
Polisi imeshinda mechi mbili za kwanza, mzunguko wa pili wa ligi dhidi ya Mtibwa Sugar na African Lyon ambapo imefikisha pointi 10.
MIKAKATI YA KUENDELEZA MPIRA WA MIGUU KWA WANAWAKE

Utangulizi:
Awali
ya yote napenda kuchukua nafasi hii kwa niaba ya kamati ya utendaji ya
TWFA kuwashukuru wajumbe wa mkutano mkuu kwa kutupa ridhaa ya kuongoza
chama kwa kipindi cha miaka minne.
Pia
napenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru wadau wote wa mpira wa miguu
kwa kutuwezesha kufika hapa tulipo. Napenda niwashukuru wadau wote kwa
ujumla wao na pia kuishukuru serikali kwa namna ya pekee zaidi kwa
mchango wake ,na mashirika na makampuni ambayo yamekuwa karibu sana nasi
NMB, SERENGETI, NSSF, PPF, na Bakheresa Group of Companies.
Tunaamini
kabisa kuwa vyombo vya habari ni washirika wetu wakubwa katika
kuendeleza mpira wa miguu wanawake. Napenda kuvishukuru vyombo vyote vya
habari hapa nchini na hata vile vya nje vilivyoweza kutoa nafasi katika
ujenzi wa mpira wa miguu wanawake.
Maendeleo ya mpira
Kutekeleza na kuendeleza mpango wa grassroot.
Kwa
kushirikiana na Shirikisho la Mpira wa miguu Tanzania,Chama cha Mpira
wa Miguu wanawake na vyama vya mikoa na wadau mbalimbali tutaendelea
kuendeleza mradi wa mpira wa miguu kwa watoto wa kike na wa kiume
Grassroot programme.(umri wa miaka 06-12).kwa mwaka 2013 mradi huu
utatekelezwa katika mikoa mitano (5) mikoa hiyo ni
Tanga,Pwani.Mwanza,Mtwara na Lindi. Mradi huu unaendeshwa kupitia shule
za msingi.Kwa mwaka 2012 Mradi huu umeendeshwa katika mkoa wa Dar es
Salaam na watoto wapatao 8766 (wasichana 4909 na wavulana 3857 ) na
walimu 26 wameshirikishwa.
Mafunzo ,semina na makongamano
Kwa mwaka 2013 tunatengemea kuendesha mafunzo mbalimbali katika nyanja kuu nne za maendeleo ya mpira wa miguu yaani Utawala na uongozi,Ualimu(Ukocha) Uamuzi na utabibu katika mpira wa miguu .Katika
mwaka mwaka 2013 mafunzo yatafanyika zaidi katika nyanja ya uongozi ili
kuwajengea stadi za uongozi viongozi wengi ambao wameingia madarakani
katika chaguzi zilizofanyika kwa mwaka 2012/2013.Mafunzo ya utawala na
uongozi yatafanyika katika mikoa nane:Dar es
Salaam,Pwani,Morogoro,Mwanza, Musoma,Shinyanga,Kilimanjaro na
Tanga.Katika mafunzo hayo baadhi ya washiriki watateuliwa kutokana na
uwezo wao kwa kuzingatia vigezo vitakavyowekwa na watahudhuria semina
itakayo andaliwa kwa kushirikiana na shirikisho la mpira wa miguu
Tanzania.
Mafunzo kwa walimu katika ngazi mbalimbali na uratibu wa utekelezaji wa mafunzo yaliyofanyika yatapewa kipau mbele.
Mafunzo
kwa waamuzi yatalenga zaidi kuibua vipaji vya watoto wa kike walioko
mashuleni na wachezaji wanaomaliza/waliomaliza muda wao.Mafunzo
yatafanyika kwa awamu mbili katika mkoa wa Dar es Salaam.
Madaktari wa michezo ni
muhimu sana katika maendeleo ya mpira na afya za wachezaji kwa
kushirikiana na vyombo husika mafunzo kwa mwaka 2013 yatafanyika kwa
awamu mbili na yatafanyika katika mkoa wa Dar es Salaam.
Wanahabari
wenye uweledi katika mpira wa miguu wa wanawake ni chachu ya maendeleo
ya mpira huo.Nafasi ya wanahabari ni kubwa katika kuendeleza mpira wa
miguu ili kuwajengea ujuzi zaidi kutakuwa na mafunzo kwa wanahabari
yatakayofanyika Dar es Salaam.
Uongozi na utawala bora
Maendeleo
ya mpira wa miguu kwa wanawake yanahitaji viongozi bora na waliopewa
ridhaa na vyombo husika.Chaguzi zimefanyika katika mikoa 16 kati 25
ya mikoa ya Tanzania Bara. Pia tunahimiza mikoa ambayo haijafanya
uchaguzi ifanye chaguzi mapema. Mikoa hiyo ni: Dar es salaam, Mwanza,
Kilimanjaro, Rukwa, Arusha, Geita, Simiyu, Njombe, Katavi na Mbeya.
Katika chaguzi hizo kuna baadhi nafasi zote hazikujazwa ni matumaini yetu kuwa zitajazwa katika mikutano ijayo ya vyama husika.
Pia
nichukue nafasi hii kuwahamasisha kina mama wengi wenye sifa kujitokeza
kugombea nafasi mbalimbali katika vyama vya mikoa na taifa pale
uchaguzi utakapoitishwa.
Mashindano
Mashindano
mbalimbali ndio moyo wa mpira wa miguu bila mashindano hakuna
anayeweza kutambua ubora na kiwango chakena pia ni kipimo cha
maendeleo.
Kutakuwa na mashindano mbalimbali katika ngazi ya mikoa,taifa na kimataifa.
Mashindano hayo pia yatahusisha shule za msingi na sekondari na
vyuo mbalimbali.Kwa kushirikiana na vyombo husika kutakuwa na
ufuatiliaji wa karibu wa michezo ya UMISSETA toka ngazi ya mkoa hadi
Taifa na kuwa na mpango endelevu wa kuwaendeleza wale wenye vipaji ambao
wamechaguliwa /wanaweza kuchaguliwa kwenye timu za taifa.
Ligi itachezwa katika ngazi za mikoa na baadaye kuunda kombaini ya mkoa itakayoshiriki mashindano ya taifa.
Kwa
mwaka 2013 tunatengemea mikoa kuchezesha ligi isiyopungua timu tano kwa
mikoa 15 itakuwa na timu 10 na timu itaruhusiwa kusajili wachezaji 25
kwa mwaka 2013 tunatengemea watoto/wasichana 3750 kushiriki katika
mpira wa miguu. Idadi hii ukizidisha mara nne unapata jumla ya
wachezaji 15,000.Endapo tutakuwa na benki ya wachezaji hawa tutaweza
kuunda timu bora za umri tofauti na zenye kiwango cha juu.
Pia
mikoa inahimizwa kuanzisha mashindano mbalimbali yatakayoamsha ari kwa
watoto wa kike na wasichana kushiriki katika mpira wa miguu.
Uratibu wa mikoa
Wajumbe
wa kamati ya utendaji pamoja na majukumu yao kama wajumbe watakuwa na
jukumu la kuratibu shughuli za maendeleo ya mpira wa miguu katika
mikoa:Uratibu huo utakuwa kama ifuatavyo:
Rose Kissiwa
|
Makamu Mwenyekiti
|
Tabora, Dodoma, Rukwa, Kigoma, Pwani
|
Amina Karuma
|
Katibu
|
Lindi, Mtwara, Iringa, Njombe, Ruvuma
|
Zena Chande
|
Mjumbe
|
Dar es Salaam, Morogoro, Katavi, Shinyanga, Mbeya
|
Triphonia Temba
|
Mjumbe
|
Manyara, Arusha, Kilimanjaro, Tanga, Singida
|
Sophia Charles
|
Mjumbe
|
Mara, Kagera, Simiyu, Geita, Mwanza
|
Kwa mujibu wa katiba ya TWFA ibara ya 37 inatoa
nafasi kwa kamati ya utendaji kuunda kamati ndogo za kuendeleza mpira
wa miguu wanawake kamati hizo ni kamati ya Fedha na mipango,kamati ya
Ufundi,kamati ya ngingine itakayoonekana inafaa.Kamati ya utendaji kwa
pamoja ilikubaliana kuunda kamati ya habari na masoko.
Kamati ya Fedha na Mipango
1. Rose Kissiwa - Mwenyekiti
2. Evans Aveva
3. Sophia Tigalyoma
4. Sophia Mukama
5. Asha Baraka
Kamati ya Ufundi
1. Tryphonia Temba – Mwenyekiti
2. Florence Ambonisye
3. Miraji Fundi
4. Dr. Leonia Kaijage
5. Furaha Francis
6. Richard Muhotoli
Kamati ya Habari na Masoko
1. Zena Chande – Mwenyekiti
2. Beatrice Mgaya
3. Mohamed Mkangara
4. Florian Kaijage
5. Somoe Ng’itu
Masoko na Habari
Mpira
wa miguu wanawake hauna udhamini na pia vyanzo rasmi vya kupata
mapato.Kwa kupitia kamati ya habari na masoko ,tunaamini kutakuwa na
mikakakti mbalimbali ya kuelimisha ,kuhamasisha wadau na watanzania wote
kuwiwa na kujitoa kuendeleza mpira wa miguu .
No comments:
Post a Comment